Exodus 28:15-20

15 a“Fanyiza kifuko cha kifuani kwa ajili ya kufanya maamuzi, kazi ya fundi stadi. Kitengeneze kama kile kisibau: cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, cha kitani safi iliyosokotwa. 16Kitakuwa cha mraba, chenye urefu wa shibiri moja
Shibiri moja ni sawa na sentimita 22.
na upana wa shibiri moja, na kikunjwe mara mbili.
17 cKisha weka safu nne za vito vya thamani juu yake. Safu ya kwanza itakuwa na akiki, yakuti manjano na zabarajadi; 18katika safu ya pili itakuwa na almasi, yakuti samawi na zumaridi; 19safu ya tatu itakuwa na hiakintho, akiki nyekundu na amethisto; 20 dna safu ya nne itakuwa na krisolitho, shohamu na yaspi. Yote yatiwe kwenye vijalizo vya dhahabu.
Copyright information for SwhKC